Wednesday, October 30, 2013

TANGANYIKA ONE: WAASI WA M23 WAONDOLEWA NCHINI DRC

TANGANYIKA ONE: WAASI WA M23 WAONDOLEWA NCHINI DRC:



Wanajeshi wa DRC wakishirikiana na jeshi la UN
linaloongozwa na wanajeshi wa Tanzania wamefanikiwa kuwaondoa waasi wa
M23 kutoka katika ngome yao kuu katika eneo la Bunagana mpakani na Uganda
 Mji wa Bunagana umekombolewa
kufuatia makabiliano makali adhuhuri ya jana ambapo baadhi ya waasi
walilazimika kuimbilia msituni huku baadhi yao wakidai waliingia Uganda wakiwa wamevalia mavazi ya kiraia
    
Msemaji wa serikali alisema kuwa mji wa Bunagana ulio katika mpaka wa Uganda na DRC, sasa uko chini ya wanajeshi wa serikali.

 .




Hatua hii ya wanajeshi ni sehemu ya ushindi
mkubwa ambao wanajeshi wamekuwa wakiupata dhidi ya waasi hao wa M23
wanaopambana dhidi ya serikali ya DRC  huku wakidaiwa
kusaidiwa na serikali ya Rwanda.







 Umoja wa Mataifa umesema kuwa wakimbizi elfu tano wamelazimika kutoroka Bunagana na kuingia Uganda kwa usalama wao.

Friday, October 11, 2013

Sunday, July 7, 2013

MALI YAONDOA HALI YA HATARI


 

Mali imeondowa hali ya hatari Jumamosi(06.07.2013) iliokuwa imedumishwa kwa miezi sita nchini humo ili kuruhusu kuanza kwa kampeni ya uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika tarehe 28 mwezi wa Julai. 

Agizo la kuweka muda maalum kwa watu kutoka nje na kupiga marufuku mikusanyiko ya watu lilianza kutumika tarehe 12 Januari siku moja baada ya Ufaransa kufanya shambulio la ghafla la kijeshi kulisaidia jeshi dhaifu la Mali kuwatimuwa wapiganaji wa itikadi kali za Kiislamu waliokuwa wamelidhibiti eneo la kaskazini mwa nchi hiyo kwa miezi tisa.

Hatua hiyo ya mkoloni wa zamani wa Mali ilikuja wakati wanamgambo wa itikadi kali za Kiislamu wenye mafungamano na kundi la Al Qaeda wenye kushikilia miji muhimu ya kaskazani walipokuwa wanasonga mbele kuelekea katika mji mkuu wa Bamako.

Mali ilikuja kutumbukia kwenye mzozo wa kisiasa baada ya mapinduzi ya mwezi wa Machi 2012 yaliofanywa na wanajeshi waliokuwa wamekasirishwa kutokana na kutimuliwa kwao kutoka maeneo ya kaskazini na makundi ya waasi ambapo walimlaumu Rais Amadou Toumani waliyempinduwa kwa kushindwa kwao.

Kuondolewa kwa hali hiyo ya hatari kunakuja baada ya jeshi la Mali hapo Ijumaa kuingia kwa amani katika mji wa mwisho uliokuwa ukishikiliwa na waasi.
Wakiandamana na wanajeshi wa Ufaransa na maafisa wa Umoja wa Mataifa, wanajeshi na wanamgambo 200 wa Mali waliingia katika mji wa Kidal ulioko mbali kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

CHANZO: DW