Mali imeondowa hali ya hatari Jumamosi(06.07.2013) iliokuwa imedumishwa
kwa miezi sita nchini humo ili kuruhusu kuanza kwa kampeni ya uchaguzi
wa rais uliopangwa kufanyika tarehe 28 mwezi wa Julai.
Hatua hiyo ya mkoloni wa zamani wa Mali ilikuja wakati wanamgambo wa itikadi kali za Kiislamu wenye mafungamano na kundi la Al Qaeda wenye kushikilia miji muhimu ya kaskazani walipokuwa wanasonga mbele kuelekea katika mji mkuu wa Bamako.
Mali ilikuja kutumbukia kwenye mzozo wa kisiasa baada ya mapinduzi ya mwezi wa Machi 2012 yaliofanywa na wanajeshi waliokuwa wamekasirishwa kutokana na kutimuliwa kwao kutoka maeneo ya kaskazini na makundi ya waasi ambapo walimlaumu Rais Amadou Toumani waliyempinduwa kwa kushindwa kwao.
Kuondolewa kwa hali hiyo ya hatari kunakuja baada ya jeshi la Mali hapo Ijumaa kuingia kwa amani katika mji wa mwisho uliokuwa ukishikiliwa na waasi.
Wakiandamana na wanajeshi wa Ufaransa na maafisa wa Umoja wa Mataifa, wanajeshi na wanamgambo 200 wa Mali waliingia katika mji wa Kidal ulioko mbali kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
CHANZO: DW